Stars watua Msumbiji.


 

Stars

TAIFA Stars inayocheza na Msumbiji kesho Jumapili iliwasili jijini Maputo jana Ijumaa saa 5:50 asubuhi ikiwa na morali kubwa huku kocha Kim Poulsen akitarajia kufanya mabadiliko kadhaa kwenye safu ya ulinzi na amesisitiza kuwa wamekuja hapa kwa nguvu moja, nayo ni ushindi tu.

Kocha huyo ambaye amewasihi mashabiki kumuita Kim badala ya Poulsen, alisema amekaa na wachezaji na kila mmoja anatamani ushindi na ndo maana wamemuahidi kupambana kufa ama kupona kutetea heshima ya nchi.

Hiyo itakuwa ni mechi ya tatu ya mashindano kwa kocha huyo mpya aliyechukua nafasi ya Mdenmarki mwenzie Jan Poulsen, kwani katika mechi ya mbili za kufuzu Kombe la Dunia alifungwa mabao 2-0 na Ivory Coast ugenini kabla ya kuifunga Gambia mabao 2-1 jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo wa Msumbiji ni kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika na katika mchezo wa awali timu zilitoka sare ya bao 1-1.

Balozi wa Tanzania nchini hapa, Shanim Nyandunga aliipokea timu hiyo na kuwataka wachezaji kuhakikisha wanashinda kwa heshima yao na nchi. Stars imefikia kwenye hoteli ya 2010 LDA, na Kim alisema; “Tumekuja hapa kusaka ushindi na kuhakikisha vijana wanasonga mbele.” Hata hivyo kikosi cha Kim kitaingia uwanjani bila ya nyota wake kiungo Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ anayesumbuliwa na maumivu ya nyama za paja.

“Sure Boy amebaki Dar es Salaam kwa sababu ni majeruhi, lakini hilo si tatizo kwani wachezaji wote waliokuwepo hapa wanaweza kuziba pengo lake. Tumekuja hapa kusaka ushindi najua mechi itakuwa ngumu kwa sababu Msumbiji ni timu nzuri na watakuwa nyumbani.”

Kim atalazimika kuifumua ngome yake kutokana kurejea uwanjani kwa Aggrey Morris ambako kutamlazimisha kumtumia kama beki wa kati pamoja na Kelvin Yondani.

Shomari Kapombe atalazimika kurudi beki wa kulia hivyo kocha atalazimia kuamua kati ya Erasto Nyoni na Amri Maftah yupi anayestahili kuanza ingawa kwa Nyoni ana nafasi kubwa ya kuanza.

Kuhusu Juma Nyoso alisema; “Nyoso amebaki Dar es Salaam kama Sure Boy,” alijibu kifupi bila ya kutoa maelezo zaidi hali inayoashiria beki huyo ambaye Simba ilitishia kumtema amekalia kuti kavu.

Chanzo: Mwanaspoti

Advertisements

Posted on June 16, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika and tagged , . Bookmark the permalink. 1 Comment.

  1. I real glad to find this web site on bing, just what I was searching for : D likewise saved to bookmarks . 863320

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: