Rafael asaini mkataba mpya Man Utd.


Rafael

Mchezaji huyo wa Brazil  amekubali kuendeleza ndoto za kuichezea Man Utd kwa kusaini mkataba mpya huku ndugu yake Fabio akiwa njiani kuelekea QPR kwa mkopo.

Beki huyo wa kushoto wa Man Utd Rafael Da Silva Amesaini mkataba mpya na Klabu hiyo utakaomfanya akae klabuni hapo mpaka mwaka 2016 kulingana na alivyosema msemaji wa mchezaji huyo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye alijiunga na Man Utd akitokea Fluminense mwaka 2008 ameweza cheza mechi 12 katika klabu ya hiyo ya Man Utd katika msimu uliopita na kumpelekea mchezaji huyo kuitwa katika kikosi cha taifa.

Msemaji wa mchezaji huyo alisema, “Rafael anafuraha ya kubakia Man utd ambayo ni miongoni mwa kalabu kubwa duniani na siku zote huwa inajihusishaga (inacheza) mechi kubwa za barani ulaya. Man Utd ndio wamekuza jina la mteja wangu na kumfanya nae kipaji chake kizidi kukuwa kwa hiyo kusaini mkataba mpya lilikuwa swala la kutolifikiria kabisa”.

Pacha wa Rafael yeye yuko mbioni kujiunga na QPR na inasemekana amekataa ofa za timu nyingine zilizopo barani ulaya ili aweze bakia hapo Uingereza ili azoee ligi hiyo.

Chanzo: Goal.com

Advertisements

Posted on June 16, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: