Kigi ndani ya Msimbazi


Kigi

SIMBA inaanza mazoezi ya uwanjani rasmi leo Jumamosi, lakini habari njema kwa mashabiki wa klabu hiyo ni kwamba Kigi Makassi jana Ijumaa alianza mazoezi ndani ya uzi mwekundu huku Ally Mustapha Barthez akisema amenogewa na Yanga alikosaini kuliko angeendelea kukaa Msimbazi.

Kigi aliyekuwa Yanga alianza mazoezi hayo ya pamoja na Simba katika gym ya Oil Com Chang’ombe jijini Dar es Salaam chini ya kocha msaidizi, Richard Amatre na alipokewa vizuri na wachezaji wenzake akionekana mwenye furaha muda wote huku wenzie wakimtania kwa kumwambia “karibu jembe.”

Alifanya mazoezi ya viungo wakibadilishana mashine na wachezaji wengine kwa ustadi, lakini hakutaka kuzungumza ujio wake Simba kwa madai bado ni mapema na alitaka afanye kazi kwanza.

Meneja wa Simba ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa kikosi hicho, Nico Nyagawa alimzungumzia Kigi na kusema: “Ni mchezaji mzuri na naamini ataisaidia Simba.”
“Kigi ni mzuri, ila anachotakiwa ni kujitambua na kufahamu majukumu yake kwa kufanya kazi ipasavyo,”alieleza Nyagawa.

Kigi ana uwezo wa kucheza winga ya kushoto kwa ufasaha pamoja na ushambuliaji wa kati, lakini pia alionyesha kiwango cha juu kucheza beki ya kushoto alipokuwa na kikosi cha timu ya taifa ya vijana U-20 kipocheza na Cameroon mechi ya kuwania kufuzu fainali za vijana Afrika.

Ujio wa Kigi kikosini hapo umeongeza nguvu kwa wachezaji wengine wapya ambao ni Mcongo Kanu Mbiyavanga kutoka DC Motema Pembe, Paulo Ngalema na Abdallah Juma waliokuwa Ruvu Shooting, Ibrahim Rajabu ‘Jeba’ kutoka Azam FC na Salum Kinje kutoka AFC Leopard.

Simba inabadili programu yake leo Jumamosi kwa kuanza kufanya mazoezi ya uwanjani na Amatre alisema itakuwa ni mambo ya kiufundi zaidi ingawa hawajajua bado uwanja watakaotumia.

Lakini huko Jangwani, Barthez amesisitiza kuwa alifanya uamuzi sahihi kusaini fomu za Yanga kwavile alichoshwa na benchi la Simba mpaka kwenye mechi za kirafiki. Kipa huyo amesaini Yanga kwa kitita cha Sh.18 milioini na mshahara wa Sh.800,000 kwa mwezi.

Alisema jana Ijumaa kuwa; “Sidhani kama kuna mchezaji ambaye anapenda kukaa benchi pasipo kucheza kikosi cha kwanza, kama yupo basi huyo hajui maana. Nilipenda kucheza kikosi cha kwanza lakini nafasi hiyo sikuipata, sikuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana na matokeo na kuondoka.

Kaseja (Juma) ni kipa mzuri, binafsi namkubali, yupo kwenye fomu, kufahamu hilo ilinisaidia na kujisikia kawaida tu,” alisema Barthez ambaye ataanza kuonekana ndani ya uzi wa Yanga Jumatatu.

Aliongeza: “Siwezi fahamu kwamba nitaanza kikosi cha kwanza, nafikiri hilo litakuwa juu ya kocha atakayekuwa akitufundisha wakati huo. Ushindani upo kila mahali, kikubwa ni kujiweka fiti na kufuata yale mwalimu anayofundisha kwa lengo la kufikia mafanikio.” alisisitiza.

Kutua kwa Barthez Yanga, kumeufanya uongozi wa mabingwa hao wa Kombe la Kagame kumrejesha Mtibwa Sugar, kipa Shabaan Kado kwa mkopo. Mpaka sasa Yanga imeshawasajili wachezaji sita wapya; Kelvin Yondan ‘Vidic’ na Ally Mustapha ‘Barthez’ (Simba), Nizar Khalfan (huru), Juma Abdul na Said Bahanuzi (Mtibwa), yosso Simon Msuva wa Moro United na Frank Dumayo (Ruvu JKT).

Hata hivyo, bado kuna utata wa Yondani kwani amesaini klabu mbili; Yanga na Simba na hivyo uamuzi wa mwisho utatolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Chanzo: Mwanaspoti

Advertisements

Posted on June 16, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: