Poulsen: Sitaki ‘anaoanao’ StarsKOCHA wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen amesema kikosi chake kimeiva tayari kwa kuiangamiza Msumbiji, hata hivyo amewataka wachezaji wake waachane na na utamaduni wa kukaa na mpira mguuni muda mrefu.

Taifa Stars ikakabiliana na Msumbiji(Mambas) katika pambano la marudiano kusaka nafasi ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika litakalopiwa Juni 17 kwenye Uwanja wa Zampeto Jiji la Maputo.
Kim alisema jana kuwa hafurahishwi na utamaduni wa baadhi ya wachezaji kukaa na mpira muda mrefu akisema aina hiyo ya uchezaji inatoa fursa kwa wapinzani kujipanga.

“Kwa ujumla naweza kusema tupo tayari kwa mapambano na kuishinda Msumbuji na kusonga mbele, tumefanya mazoezi mepesi lakini hasa nilikuwa nakazania ufungaji.

“Nimewambia wachezaji wangu hakuna sababu ya kukaa na mpira muda mrefu, Samata(Mbwana) amekua tabia ya ‘anaoanao’ mpira, matokeo yake anachoka,”alisema Kim.

“Nataka mchezaji anapopata mpira aangalie kisha atoe pasi na kufungua kama anavyofanya Boban(Haruna). Yeye ni mfano mzuri akipata mpira anaangalie kisha anapiga pasi sehemu husika,”.

Aidha, Mdenmark huyo alisema kuwa, kurejea kwa baadhi ya wachezaji wake waliokuwa majeruhi akiwamo Nurdin Bakar, Shaaban Nditi na beki Aggrey Morris kumeongeza nguvu katika kikosi chake.

Katika hatua nyingine, kikosi cha Taifa Stars kinatarajia kuagwa na kukabidhiwa bendera leo kabla ya kesho kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Kenya, Kenya Airways kwenda kuelekea.

Advertisements

Posted on June 14, 2012, in Mpira. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: