Mkwasa: Tuiunge mkono Twiga Stars


KOCHA Mkuu wa Twiga Stars, Charles Mkwasa amewataka Watanzania kuiunga mkono timu hiyo katika mechi ya marudiano dhidi ya Ethiopia kama walivyofanya kwa Taifa Stars ilipovaana na timu ya taifa ya Gambia kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kushiriki Fainali za Kombe la Dunia 2014.

Mkwasa alisema wachezaji wa Twiga Stars wakiungwa mkono watapata hamasa kubwa na kupigana kwa nguvu zaidi katika kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo huo ambao ni muhimu kushinda ili ishiriki kwenye Fainali za Afrika kwa Wanawake zitakazopigwa mwaka huu huko Guinea ya Ikweta.

Twiga Stars itashuka dimbani Jumamosi ijayo huku ikiwa na kumbukumbu ya kutandikwa mabao 2-1 na Ethiopia katika mchezo wa kwanza uliopigwa Addis Ababa.

Mkwasa alisema kuwa kikosi chake kipo vizuri na wanaendelea kujifua vilivyo kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Alisema kutokana na maandalizi waliyoyafanya kwa ajili ya mchezo huo ana matumaini ya kufanya vizuri na amewataka Watanzania kuiunga mkono timu hiyo kama ilivyo kuwa kwa Taifa Stars ilipocheza na Gambia wiki iliyopita.

“Tunaendelea vizuri na maandalizi yetu vijana wapo katika hali nzuri hivyo nina matumaini makubwa kuwa watafanya vizuri kwenye mechi yetu ya marudiano dhidi ya Ethiopia.

“Mapungufu yote yaliyojitokeza kwenye mechi yetu ya kwanza kwa hakika tumeshayafanyia kazi hivyo Watanzania wote naomba wawasapoti vijana wetu ili wafanye vizuri kwenye mchezo huo kama ilivyokuwa kwa Taifa Stars,” alisema Mkwasa.

Twiga Stars inahitaji ushindi wa bao 1-0 ili ikate tiketi ya kushiriki kwenye fainali hizo na itakuwa ni mara yake ya pili kutinga katika hatua hiyo, ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2008.
Chanzo Mwananchi

Advertisements

Posted on June 14, 2012, in Bongo, Mpira, Mpira kwa Dakika, Shuti la leo. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: