Juve wamtuma Nedved kwa Van Persie..


ROBIN VAN PERSIE

Timu ya Juventus amemtuma mkurugenzi wake wa michezo ambaye pia alikuwa mchezaji wao wa zamani Pavel Nedved kwenda kukutana na Robin van Persie kwa ajili ya kumshawishi ajiunge na timu hiyo ya Italia.

Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Czech alitumwa na Juve kwenda katika kambi ya timu ya Uholanzi ambayo ipo katika mashindano ya Euro kwa ajili ya kuongea na van Persie ili aweze jiunga na klabu ya Juve.

Mabingwa hao wa Italia wanataka Van Persie ndo awe mchezaji wao muhimu ambaye wanahitaji msajili katika kipindi hiki cha usajili na wako tayari kutoa ada ya paundi mill 25 na mshahara wa paundi 180,000 kwa wiki.

Klabu nyingine inayomtaka mchezaji huyo ni Man City na klabu hiyo pia wanaweza fikia viwango hivyo vya fedha sema tatizo linakuja kama watamtaka van Persie basi itabidi wachezaji wengine wauzwe na wachezaji watakaokuwa hatiani hapo kuuzwa ni Tevez na Dzeko.

Arsenal wamempa mkataba van Persie wa miaka mitatu ambao atakuwa akipokea paundi 130,000 kwa wiki lakini mpaka sasa mchezaji huyo hajasaini mkataba huo na mwisho wake mpaka sasa haujajulikana.

Chanzo: Dailymail

Advertisements

Posted on June 14, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: