Bendtner matatani.. Kisa chupi..!


Bendtner

Mchezaji wa timu ya taifa ya Denmark ameingia matatani  baada ya kuonekana kwa chupi yake pindi alipokuwa akishangilia.

Bendtner amedai ya kuwa alikuwahajui kama anavunja sheria kwa kuonesha chupi hiyo, chupi ambayo anaisema ni chupi yake ya bahati.

Mchezaji huyo alifunga magoli mawili dhidi ya Ureno na katika kushangilia kwake aliishusha bukta yake na kupandisha flana ili kuonesha chupi yake hiyo ya bahati.

Chama cha mpira cha Denmark kimemgombeza mchezaji huyo kwa kitendo hicho kwani alikuwa anaitangaza kampuni ya Paddy Power. Huku kampuni hiyo haina mkataba na chama hicho.

” Ni chupi tu ya kawaida, ambayo ambayo kila nkiivaa  basi huwa nafunga magoli, nimeivaa tokea mechi ya kwanza ya mashindano ya Euro na hata kabla ya mashindano hayo. Lakini nlikuwa sijui kama kuionesha chupi hiyo ni kuvunja sheria lakini sasa namegundua na sitorudia”.

Lakini bado UEFA inaweza mhukumu mchezaji huyo kwa kitendo hicho, huku kampuni ya Paddy Power wakimshukuru mchezaji huyo kwa utangazaji huo,
“Nimefurahishwa sana na alichokifanya Nicklas, amecheza vizuri sana leo ni bahati mbaya tu wamefungwa lakini kutokana na kuvaa chupi zetu ameweza funga magoli mawili safi kabisaa” alisema Ken Roberto wa kampuni ya Paddy Power.

Chama cha mpira cha Denmark ambacho kinadhaminiwa na kampuni ya Ladbrokes nacho kikasema, “Tumeongea na mchezaji (Bendtner) na kuanzia leo hatovaa chupi hiyo katika mechi zijazo”

Chanzo: Dailymail

Advertisements

Posted on June 14, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: