Hodgson: Sikumchagua Rio sababu mchezaji kama yeye hawezi kukaa benchi


Rio: Atarudi timu ya uingereza baada ya Mashindano ya Ulaya 2012 kuisha

Bosi wa timu ya Uingereza, Roy Hodgson amesema alikasirishwa na maneno juu ya uamuzi wake wa kumuacha Rio Ferdinand kwenye kikosi chake, na amesisitiza kuwa jamaa bado ana kipaji kizuri mbeleni..

Kuachwa kwa Rio kwenye kikosi hicho kilishangaza wengi na baada ya kuachwa kwa Cahill bado Hodgson hakumfata Rio.

Mwakilishi wa Rio, Jamie Moralee, aliishutumu Chama cha mpira cha Uingereza pamoja na Hodgson kutokana na kumdharau Rio na kusema sababu za kimpira hazikuwa sababu maalum.

Lakini Hodgson ameeleza kwann alienda kwa mchezaji wa Liverpool Martin Kelly badala ya kwenda  kwa Rio.

‘Nilishangazwa baada ya kuona maneno yameanza tena’, alisema Hodgson. ‘Kinachoshangaza kwa sisi tunaofanya kazi hapa ni kupoteza mwelekeo wetu kwenye mechi kubwa na Ufaransa inayotukabili jumatatu ‘.

‘Sidhani kama Rio ni mchezaji unayemchagua kuziba nafasi ya mchezaji mwingine. Nadhani unapomchagua Rio pamoja na udhohefu wake, unamchagua kuja kumuweka kwenye kikosi.’

‘Mawazo yangu, yalienda kwa mchezaji mdogo ambaye tunaweza kumuweka na akaweza kufaidika. Tulienda kwa Martin Kelly ambae tulikuwa nae nyuma kwenye safari ya Norway’.

‘Jina la Rio halikuwepo kwenye mjadala’.

Ferdinand amekosa matumaini ya kucheza na timu hiyo, ila Hodgson anasisitiza atamwita pindi mashindano ya UERO yatakapoisha.

Hodgson amesema ‘Ferdinand asijali kuhusu future ya mpira wake. Muda wote atakaoendelea kucheza, nitaendelea kumuangalia’.

Advertisements

Posted on June 10, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: