Maxi bado nipo Liver..


Maxi Rodriguez

Maxi Rodriguez amekanusha habari zakuwa ameihama Klabu ya Liverpool na kuJiunga na Klabu ya Newell’s Old Boys ambayo ipo Argentina.

Kiungo mshambuliaji huyo alikuwa anatarajiwa kuondoka Liverpool mwisho wa msimu huu baada ya kuweza cheza mechi 21 tu na karibia zote alikuwa akitokea benchi katika msimu wa 2011/12.

Maxi amebakiza miezi 12 katika mkataba wake na alionekana akiwaaga mashabiki wa Liverpool mwisho wa msimu katika mechi ya mwisho wa msimu  iliyofanyika Anfield dhidi ya Chelsea.

Hivi karibuni alionekana mjini Rosario na ikasemekana amejiunga na Klabu ya Newell’s lakini Maxi  alikanusha habari hizo na kusisitiza kuwa sio za ukweli.

“Sijui hizo habari zinatokea wapi, Mie nimebakiza mwaka mmoja mzima katika mkataba wangu na Liverpool na wala sijaongea na yeyote kuhusu maswala ya kuhama” alisema Maxi.

Kuondoka kwa Dalglish na kuchaguliwa kwa Brendan Rodgers kutawapa wachezaji wengi mwanzo mpya ambao katika kipindi cha Kenny maisha yao yalikuwa magumu Klabuni hapo.

Chanzo: Skysports

Advertisements

Posted on June 8, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: