Clarke kocha West Brom.


Clarke

Steve Clarke ametangazwa kuwa Kocha wa timu ya West Brom Albion.

Timu hiyo imekuwa ikitafuta kocha baada ya kocha wao Roy Hodgson kuchaguliwa kuwa kocha wa timu ya taifa.

Aliyekuwa kocha msaidizi wa Liverpool Steve Clarke ndio amepewa timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili.

“Ninafuraha sana kupewa nafasi hii, kuwa kocha mkuu ni kitu ambacho nimekuwa nikikitaka tokea zamani. Nimejaribu kufanya kila niwezalo kama kocha msaidizi huku nkisaidiana na makocha tofauti tofauti duniani na nimeweza jifunza mengi sana”. Alisema Clarke.

Clarke aliondoka Liverpool jumatano kwa ajili ya kuchukua nafasi hiyo ya ukocha. Mwanzo Clarke aliandika barua ya kutaka kuacha kazi kutokana na kufukuzwa kwa Dalglish lakini barua hiyo ilikataliwa na uongozi wa Liverpool.

“Nimeweza jifunza vitu vingi toka kwa makocha (mameneja) wote ambao nimeweza fanya nao kazi, ninafurahi West Brom wamenipa nafasi hiyo ya kunifanya kuwa kitu ambacho nlikuwa nakitaka tokea mda mrefu sasa na ntajitahidi kutowaangusha”.  Alisema Clarke.

Mkurugenzi wa michezo wa West Brom nae alisema,
“Nina mkaribisha Steve katika klabu hii na tunaamini tumemchagua mtu mzuri na anaefaa kuiendesha na kuipeleka Klabu mbele”.

Chanzo: Dailymail

Advertisements

Posted on June 8, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: