Manuel Preciado afariki baada ya kupewa ukocha Villareal.


Manuel Preciado

Kocha mpya wa Villareal Manuel Preciado afariki dunia kwa kupata mshtuko wa Moyo(heart attack), kocha huyo ambaye amefariki akiwa na miaka 54 amefariki masaa 24 baada ya kukubali kuchukua mikoba iliyoachwa na El Madrigal kwa ajili ya kukinoa kikosi cha Villareal.

Preciado alikuwa kocha wa Sporting Gijon lakini Januari alifukuzwa na kubakia kuwa hana timu ya kufundisha lakini masaa 24 yaliyopita alikuwa ameshakubaliana na Villareal kuwa kocha wa Timu hiyo kabla mauti hayajamkuta. Mwaka jana mwezi wa nne Preciado na timu yake ya kipindi hicho Gijon ndo walikuwa wakwanza kuwafunga Jose na timu yake ya Madrid baada ya timu hiyo ya Madrid kucheza mechi zao kumi za mwanzo bila kufungwa.

Preciado pia ameshawahi kuzinoa timu za Racing Santander, Gimnastic, Murcia na Levante na alipokuwa mchezaji zamani alikuwa beki wa timu za Racing, Mallorca na Alaves.

Beki wa timu ya Barcelona alitoa rambirambi zake kupitia mtandao wa twitter kwa kusema, “(Preciado)Ni miongoni mwa watu bora katika mchezo huu wa mpira wa miguu.”

Fabregas nae akasema,
“Mpaka sasa nashindwa amini habari hii nliyoipata. Nawapa pole familia ya Manolo Preciado. RIP rafiki yangu.”

Klabu ya Villareal nayo aimetoa maelezo ya kuwa,
” Villareal inatoa pole kwa familia ya marehemu,ndugu na jamaa wote wa marehenu kwa pigo hilo kubwa”.

Chanzo: Caughtoffside

Advertisements

Posted on June 7, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: