England watua Poland.


England ndani ya Poland

Timu ya Uingereza imewasili Poland Jumatano na Mchezaji wa Man Utd Wayne Rooney amewaomba wachezaji wenzake wajitume kupitiliza katika mashindano hayo.

Nahodha na kiungo wa England,Steven Gerrard

Wachezaji wengi wa Timu hiyo wanakubali ya kuwa timu ya taifa ya Uingereza imekuwa kituko katika mshindano mengi lakini sasa wanataka kuhakikisha heshima yao inarudi.

Krakow Airport

” Najua sie kama wachezaji, tunahitajika kufanya vizuri tofauti na miaka ya nyuma na tunaelewe ya kuwa ukichaguliwa Timu ya Taifa basi ujiandae kusemwa. Inatubidi  tujitume na tuweze shinda mashindano haya. Kama tukijitahidi halafu tukafungwa basi hapo tutatoka kifua mbele kwamba tumejitahidi hadi mwisho lakini bahati haikuwa yetu na sio kujilegeza na kutolewa kizembe. Sioni sababu ya kutufanya tushindwe chukua kikombe kwa maana wachezaji tunao naa ni wazuri. Kocha ameweza kuleta umoja katika timu na dhumuni letu ni kufika nusu fainali au hata fainali kabisa”.alisema Rooney

Mashabiki wakiwakaribisha

Rooney amefungiwa kucheza mechi mbili za mwanzo za mashindano hayo kutokana na kadi nyekudu aliyoipata wakati wakicheza dhidi ya Montenegro katika mechi za kufuzu. Lakini ataruhusiwa mechi ya tatu katika hatua ya makundi ambayo itakuwa ni dhidi ya Ukraine katika mji wa Donestk.

(mstari wa nyuma, kushoto – kulia) Andy Carroll, Phil Jones, John Terry, Rob Green, Joe Hart, Jack Butland, Joleon Lescott, Martin Kelly, Danny Welbeck (mstari wa pili) Gary Neville (coach), Ray Lweington (kocha msaidizi), Jordan Henderson, James Milner, Glen Johnson, Scott Parker, Phil Jagielka, Stewart Downing, Ray Clemence (kocha wa makipa), Dave Watson (kocha wa makipa), (mstali wa mbele) Alex Oxlade-Chamberlain, Jermain Defoe, Theo Walcott, Steven Gerrard, Roy Hodgson (meneja), Wayne Rooney, Ashley Cole, Ashley Young, Leighton Baines .

 

Chanzo: Dailymail

Advertisements

Posted on June 7, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: