Ronaldo: Ntamalizia mpira wangu Madrid.


Ronaldo

Christiano Ronaldo amefutilia mbali uwezekano wa kuweza kurudi tena Uingereza baada ya kusema ana mpango wa kumalizia mpira wake Madrid.

Mchezaji huyo wa Madrid ameweza funga magoli 60 katika mechi 55 ndani ya msimu huu ulioisha. Kati ya hayo magoli 46 ni ya Ligi na kuweza kuisaidia Madrid kutwaa kombe.

Ronaldo aliyenunuliwa kwa ada ya paundi mill 80 akitokea Man Utd, ameonesha nia ya kubakia Madrid milele,
“Kuna kipindi huwa nafikiriaga swala la kuwa mie ndo mchezaji ambaye nimenunuliwa kwa bei kubwa mpaka sasa dunia nzima na hilo hunifanya njitume sana nkiwa uwanjani. Kuhusiana na mkataba wangu na Madrid, kwa upande wangu mie ngependa kukaa na Klabu hii mpaka ntakapo staafu soka. Sisemi hivi kwa utani ila namaanisha nkisemacho nataka kumalizia soka langu hapa Madrid. Ngependa hata kusaini mkataba wa miaka kumi 10 lakini ni swala la maamuzi ya pande mbili sio ya kwangu tu”. Alisema Ronaldo.

Mchezaji huyo toka Ureno amefurahiswa na kocha wake Jose Mourinho kusaini mkataba mpya ambao utaisha mwaka 2016 na anatamani Mourinho abakie nae hapo Klabuni kwa mda mrefu nae.

Chanzo: Talksport

Advertisements

Posted on June 6, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: