Barton avamiwa akiwa Liverpool.


Joey Barton apigwa

Mchezaji wa timu ya QPR Joey Barton amepata majeraha baada kupigwa usoni na watu wawili nje ya  Klabu ya muziki iitwayo Garlands ambayo ipo jijini Liverpool.

Mchezaji huyo ambaye ambaye nafasi yake QPR ipo mashakani amehusika katika ugomvi huo kwa kupigana na wanaume wawili kabla ya ugomvi kuamuliwa na polisi.

Picha katika mtandao wa Twitter unaonesha polisi na mwanamke wakimzuilia Barton asiendele kupigana.

Polisi mmoja wa Merseyside (Liverpool) alisema, ” Polisi wa Merseyside waliitwa kwenda mtaa wa Eberle mjini Liverpool saa 5:30 alfajiri baada ya kupewa taarifa ya fujo. Walipofika walimkuta Mwanaume mwenye umri wa miaka 29 (Barton) akiwa na majeraha usoni lakini mtu huyo aliondoka haraka sana bila ya kujulikana alikokimbilia.
Watuhumiwa wengine waliokuwa wakipigana na mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 29 wote wawili wametiwa mbaroni kwa kusababisha fujo mtaani”.

Barton (kulia)

Pamoja na matatizo yote ambayo Barton ameyapata ya kufungiwa mechi 12 za ligi kutokana kuwapiga Tevez, Aguero na Kompany lakini bado mchezaji huyo hajakoma na kuendelea kufanya fujo hadi nje ya uwanja.

Mchezaji huyo ameshawahi kufungwa jela kwa mda wa miezi sita (6) baada ya kusababisha fujo katikati ya jiji la Liverpool. Pia wakati anaichezea klabu ya Man City alishawahi tozwa faini ya Paundi 60,000 kwa kosa la kumchoma sigara jichoni mchezaji mwenzake wa hapohapo Man City Jamie Tandy.

Chanzo: Dailymail 

Advertisements

Posted on June 4, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: