Fenerbahce wamsajili Kuyt.


Dirk Kuyt

Timu ya Fenerbahce imetangaza ya kuwa imemsajili mshambuliaji wa Liverpool Dirk Kuyt kwa mkataba wa miaka mitatu (3).

Timu hiyo ya Uturuki inaaminika imetoa kiasi cha paundi mill1 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye asili ya Uholanzi.

Uhamisho wa Kuyt umekuwa ukizungumziwa kwa mda mrefu sasa baada ya mchezaji huyo kutokuwa na nafasi katika timu hiyo. Katika mechi nyingi amekuwa akitokea benchi na hiyo pekee imetosha kupelekea kuondoka kwa Kuyt.

Kuyt alikuwa amebakiza mkataba wake wa mwisho Liverpool na kocha mpya wa Liverpool Brendan Rodgers ameamua kumuachia Kuyt ahamie Timu nyingine ili aweze pata mda zaidi wa kucheza na sio kutokea benchi.

Klabu nyingi zilimtaka Kuyt zikiwemo klabu za Fenyenoord na Hamburg, klabu hizo zilionesha dhamira ya kumtaka Kuyt lakini Fenerbahce wameweza wapiku.

Kuyt amekaa Liverpool kwa mda wa miaka sita 6, hii ni tokea alipohamia klabuni hapo akitokea Feyenoord mwaka 2006 kwa ada ya paundi mil 10. Amecheza mechi 276 na kuweza funga magoli 71 akiwa klabuni hapo (Liverpool).

Kuyt alifunga goli katika fainali ya Carling Cup dhidi ya Cardiff msimu ulioisha na kumfanya awe amenyakua kombe moja tu akiwa na Klabu hiyo.

Chanzo: Skysports

Advertisements

Posted on June 3, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: