Taarabt : sitaki cheza na Barton.


Adel Taarabt (kushoto) na Barton (kulia)

Mchezaji wa timu ya QPR Adel Taarabt ameongeza Presha katika timu hiyo baada ya kusema hataki kucheza tena pamoja na kiungo Joey Barton.

Barton (kulia)

Barton alijiharibia mwenyewe katika mechi yao ya mwisho ambayo walicheza na Man City. Mchezaji huyo alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kiwiko Tevez na  kugawa dozi zaidi kwa Aguero na Vicent Kompany na kusababisha kufungiwa mechi 12 za msimu ujao.

QPR watafanya uchunguzi wao wenyewe wa ndani kuhusiana na tabia ya Barton wiki ijayo na tayari mchezaji huyo ameshapigwa faini ya paundi 75,000 na shirikisho la mpira la Uingereza FA.

Kama QPR watataka kumfukuza mchezaji huyo basi inabidi wamlipe kiasi cha paundi mill 11 ili kufidia  fedha za mkataba waliovunja na mchezaji huyo.

Inasemekana matendo ya Barton yamesababisha utengano baina ya wachezaji na Taarabt ndo kinara kumpinga mkorofi Barton.

Taarifa za karibu zinasema, Taarabt amegoma kucheza tena na mchezaji huyo na kuwa wawili hao wamekuwa hawaongei na  miezi kadhaa sasa imepita bila hata ya salamu.

Wachezaji wote wawili wanamakubwa yao yaliwahi kuwakumba. Wote wanjiona ni bora kuliko watu wengine na hii yapelekea kutoweza elewana kwa wawili hao.

Barton matatizo yamekuwa yakimfuata tokea zamani alipoamua kumchoma mchezaji mwenzake James Tandy jichoni pindi wakati wote ni wachezaji wa Man City.

Taarabt nae alitoa mpya baada ya kugoma kurudi uwanjani katika kipindi cha mapumziko baada ya timu yake ya QPR kufungwa magoli 6-0 na Fulham.

Barton alimsemea mbovu mchezaji huyo kwamba,
“Nlipowasili hapa QPR nliambiwa Taarabt ni mchezaji mzuri lakini mpaka sasa sijaliona hilo. Sijui labda ni kwasababu ni mvivu tu, hapendi jituma.”

Kwa hiyo kocha wa QPR Mark Hughes anauamuzi mgumu mbele yake wa kuamua aidha ampoteze Barton au Taarabt.

Chanzo: Dailymail

Advertisements

Posted on June 2, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: