PSG wamtaka rooney kwa Paundi mill 100.


Wayne Rooney

PSG wameandaa kitita cha paundi millioni 100 ili kumsajili mshambuliaji wa Man Utd Wayne Rooney.

Fedha sio tatizo kwa Klabu hiyo ambayo imemaliza ya pili katika ligi ya Ufaransa msimu uliopita na Kocha wa Timu hiyo memtaja Rooney kama ndo mchezaji anayemuhitaji ili kuipeleka Klabu hiyo mbele kimafanikio.

Habari zaidi zasema Messi ndo alikuwa chaguo la kwanza lakini baada ya kuona itakuwa ni ngumu kumpata mchezaji huyo sasa PSG wamehamia kwa Rooney.

Rooney aliandika barua ya kutaka kuhama Old Trafford Oktoba 2010 lakini mara ghafla akasaini mkataba mpya mara baada ya kuongea na Ferguson.

Rooney sasa haoneshi dalili yoyote Man Utd na ameweza  fanikiwa kufunga magoli 27 msimu huu ulioisha, kwa hiyo itakuwa ngumu kwa PSG kuweza mlubuni Ferguson amuachia mchezaji huyo.

Hata hivyo yote yanawezekana kwa maana United walimuuza C.Ronaldo kwa R.Madrid kwa ada ya paundi mill 80 na sasa Klabu hiyo imejaa madeni kwa hiyo kupokea paundi mill 100 itakuwa ngumu kidogo kuikataa.

Chanzo: Dailymail

Advertisements

Posted on June 2, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: