Lambert awa kocha Aston Villa.


Paul Lambert

Aston Villa wamemtangaza kocha wao mpya leo ambaye ndiye aliyekuwa kocha wa Norwich, Paul Lambert.

Aston Villa walikuwa wanhausishwa na kocha huyo kwa mda mrefu sasa na inasemekana walikuwa wanakwama kwenye swala la makubaliano ya fedha za kutoa kwa ajili Aston Villa waweze mpata kocha huyo.

Klabu ya Aston Villa imetoa ujumbe usemao, ” Bodi ya Aston Villa inafuraha kutoa taarifa ya kuwa Paul Lambert amechaguliwa kuwa Kocha wa Villa”.

Alhamisi Lambert alitaka kuacha kazi ili aweze kujiunga na Villa lakini bodi ya Norwich ilikataa barua yake ya kuachia ngazi.

Lambert na Alex McLeish

Kocha huyo amepewa mkataba wa miaka mitatu (3) katika Klabu hiyo ya Villa na mashabiki wanatarajia mscotland huyo ataisaidia timu na isiwe kama ilivyokuwa wakati wa utawala wa Alex McLeish.

Itakuwa ni piga kubwa kama kuondoka kwa kocha huyo kukifuatiwa na kuondoka kwa mshambuliaji wao Grant Holt.

Mshambuliaji huyo wa Norwich inasemekana anataka nae kuihama Klabu hiyo.

Inaaminika Villa wamelipa kiasi cha paundi mill 1 kwa ajili ya kuvunja mkataba aliokuwa nao Lambert na Norwich na kumfanya kocha huyo kuwa kocha wa nne katika kipindi cha miaka miwili.

Chanzo: Dailymail 

Advertisements

Posted on June 2, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: