AC Milan kuwaweka sokoni Pato,Cassano/Boateng na Robinho.


Antonio Cassano na Zlatan Ibrahimovic

Timu ya Italia ya AC Milan italazimika kuwauza kati ya wachezaji wao (Pato,Cassano/Boateng,Robinho) ili kuweza pata fedha ya kusajili wachezaji wengine.

Milan yalazimika kuwauza wachezaji wake ili kuweza kununua wachezaji wengine ili kuifanya timu iwe imara na tayari kwa msimu wa mwaka 2012-13.
Milan imepata ofa nyingi kutoka klabu mbalimbali kwa ajili ya mshambuliaji Ibrahimovic na beki Thiago Silva lakini miamba hiyo ya Italia hawako tayari kuwapoteza wachezaji hao kwa sasa na matokeo yake itawabidi wawauze wachezaji wengine ili kuweza pata fedha za usajili.

Ingawaje wachezaji hao ambao wamewekwa sokoni ni wachezaji muhimu kwa Milan lakini Timu hiyo haina ujanja mwengine zaidi ya kuuza baadhi ya hao wachezaji ili kuweza pata fedha itakayo waruhusu kufanya usajili.

Pato anafuatiliwa kwa karibu na Klabu ya PSG ya ufaransa na Kocha wa timu hiyo C.Ancelotti anavutiwa sana na Mbrazil huyo kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa wakamchukua.

Robinho nae inasemekana anaweza rudi katika klabu yake ya zamani ya Santos, ingawaje maelewano kuhusiana bei ya kumnunulia wa mchezaji huyo ndo itakuwa kikwamisho kwa maana Milan watahitaji pesa nyingi kumuachia.

Boateng mwenye umri wa miaka 25 ananyemelewa na klabu nyingi kutoka Uingereza na uuzaji wa mchezaji huyo kutaipelekea Milan kupata fungu la kutosha.

Hakuna ofa iliyokuwa wazi kwa Cassano lakini Milan wanadhani itapatikana tu ili kuweza kumuuza mchezaji huyo na kuweka vitabu vyao vya mahesabu sawa.

Chanzo: Goal

Advertisements

Posted on May 31, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: