Scholes na Amos waongeza mkataba Man Utd.


Scholes

Man Utd wamedhihirisha ya kuwa kiungo mkongwe Paul Scholes amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja na pia kipa Ben Amos amesaini mkataba wa miaka mitatu na timu hiyo.

Scholes ambaye miezi 12 iliyopita alistaafu soka kabla ya kuamua kurudi tena uwanjani mwezi wa kwanza wa mwaka 2012.

Baada ya kurudi uwanjani Scholes aliisaidia sana timu hiyo ambako mechi yake ya kwanza aliingia akitokea benchi katika mechi dhidi ya Man City katika kombe la FA.

Scholes amefanikiwa kufunga magoli manne katika mechi 17 za ligi alizocheza tokea arudi kutoka kustaafu.

Mchezaji huyo ambaye amechezea klabu moja mpaka leo (Man Utd) ameweza kufunga magoli 154 katika mechi 697 ambazo amecheza katika klabu hiyo. Rekodi hiyo inamfanya Scholes awe namba tatu katika orodha ya wachezaji ambao wameichezea Man Utd mechi nyingi zaidi huku namba moja akiwa Sir Bobby Charlton na mbili ni Ryan Giggs.

Ben Amos

Kipa nae wa Man Utd Amos amesaini mkataba wa miaka mitatu.

Amos alicheza mechi yake ya kwanza kwa klabu hiyo Januari katika mechi dhidi ya Stoke City na vilevile alicheza katika mechi za Carling Cup.

Mchezaji huyo amekuwa kitolewa kwa mkopo mara kwa mara na kuna uwezekano mkubwa akatolewa kwa mkopo pia msimu ujao.

Chanzo: Skysports

Advertisements

Posted on May 30, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: