Liverpool wampata kocha.


Brendan Rodgers

Brendan Rogers ambaye ni kocha wa timu ya Swansea amekubali mkataba wa kuwa kocha mpya wa Liverpool FC.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 39 atasaini mkataba wa miaka mitatu (3) na klabu hiyo na kutangazwa kwake rasmi kutafanyika ndani ya masaa 24.

Liverpool itabidi iwalipe Swansea kiasi cha fedha kuanzia paundi milioni 4 mpaka 5 kutokana na kukatisha mkataba wake aliokuwa nao na timu ya Swansea city.

Rodgers ameweza kuifanya timu ya Swansea kucheza mpira mzuri na wakuvutia katika msimu wao wa kwanza katika ligi kuu, hii ni pamoja na kuwafunga Liverpool katika mechi yao ya mwisho wa msimu.

Baada ya kumuachisha kibarua Dalglish, timu ya Liverpool ilihusishwa na makocha wengi sana ambao wangechukua nafasi ya Dalglish hii ni pamoja na R.Martinez, Villa-Boas, Fabio Capello, Frank de Boer na Benitez ila kati ya wote Rodgers ndo kaibuka kinara.

Rodgers alikataa kuongea hata na wamiliki siku 12 zilizopita mwanzo alipofuatwa kwa ajili ya kumrithi Dalglish na kuwafanya wamiliki kuhamisha maongezi yao kwa Martinez lakini Rodgers alibakia kuwa chaguo la kwanza kwa Mabosi hao wa Liverpool.

Maisha ya Ukocha ya Rodgers yalianzia Watford baadae Reading na pia aliwahi kuwa hata kocha wa timu ya akiba Chelsea.
Baadae akarudi tena Reading lakini hakukaa sana na ndipo alipojiunga na Swansea 2010 na akaweza ipandisha daraja timu hiyo May 2011 na kuifanya Swansea kuwa timu ya kwanza kutoka Wales kucheza katika Premier League.

Mchezaji wa zaman wa Uingereza Gary Lineker amesema katika mtandao wa twitter kuwa,
“Nadhan huu ni uamuzi mzuri na wenye akili sana, anaujua mpira.”

Chanzo: BBC

Advertisements

Posted on May 30, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: