TFF yabariki uchaguzi Yanga


KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imekubali ushauri uliotolewa na Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ambapo imeiagiza Yanga kupitia Kamati yake ya uchaguzi kuanza mchakato wa kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wajumbe wake wa Kamati ya Utendaji.

Awali,Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji chini Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa iliyokutana Juni 26 ilitoa mwongozo kwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF ikishauri ufanyike uchaguzi mdogo ndani ya Yanga baada ya Kamati yake ya utendaji ya Yanga kukosa akidi kwa sababu wajumbe wake wengi walijiuzulu.

“Tumebaini kwamba Kamati ya Utendaji ya Yanga imekosa akidi baada ya wajumbe wake wengi kujiuzulu, hivyo kutokuwa na uwezo wa kufanya uamuzi kwa mujibu wa Ibara ya 32(1) ya Katiba ya klabu hiyo,”alisema Mgongolwa na kuongeza kuwa:

“Ili kupata akidi na kufanya uamuzi Kamati ya Utendaji ya Yanga yenye wajumbe 13 inatakiwa kuwa na asilimia 50 ya wajumbe wote, hivyo ili wafanye uamuzi halali hawatakiwi kupungua saba,”

Mgongolwa alisema wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga ambao hawajajiuzulu ni Sarah Ramadhan, Mohamed Bhinda, Tito Osoro na Salim Rupia ambao kwa hivi sasa hawawezi kufanya shughuli zozote za Yanga hadi nafasi zilizo wazi katika Kamati ya Utendaji zitakapojazwa.

Pia alisema kuwa kwa mujibu wa ibara ya 29(3) ya Katiba ya Yanga nafasi zilizo wazi katika Kamati ya Utendaji zinatakiwa kujazwa katika Mkutano Mkuu wa Kawaida ujao.

Mbali ya kutoa mwongozo huo kwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, kamati hiyo ya Mgongolwa pia iliipa sekretarieti ya Yanga chini ya Katibu Mkuu Selestine Mwesigwa mamlaka ya kuiongoza klabu hiyo katika kipindi chote kabla ya uchaguzi.

Kwa upande mwingine, taarifa ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliyotolewa jana jioni na ofisa habari wa shirikisho hilo Boniface Wambura iliiagiza Yanga kuhakikisha inaanza mchakato wa uchaguzi Juni 1 kwa kuzingatia katiba ya klabu hiyo ibara 28.

Wambura alisema Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Uchaguzi ya TFF, Deogratias Lyatto ameiagiza Kamati ya uchaguzi ya Yanga kwamba kuhakikisha uchaguzi wa kujaza nafasi zilizoachwa wazi unafanyika Julai 15 siku ambayo pia klabu hiyo itakuwa ikifanya mkutano wake mkuu wa wanachama.

Aidha Lyatto aliagiza pia mkutano mkuu wa uchaguzi wa Yanga uwe na ajenda moja tu ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi, pamoja na kuitaka Kamati ya uchaguzi ya Yanga kusimamia machakato huo kwa kuishirikisha sekretarieti ya Yanga.

Chanzo Mwananchi

Advertisements

Posted on May 28, 2012, in Bongo, Mpira, Mpira kwa Dakika, Shuti la leo. Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: