Simba waiteka Dar


Mashabiki wa Simba

MAMIA ya mashabiki wa Simba ya jijini Dar es Salaam jana walijitokeza barabarani kuishangilia timu hiyo ilipokuwa ikilitembeza kombe lao la ubingwa wa Ligi Kuu.

Msafara huo ulianza saa 7 mchana kutokea makao makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Msimbazi na kupita barabara ya Morogoro, Mandela hadi barabara ya Kilwa kuelekea kwenye ukumbi wa Dar Live Mbagala.

Katika msafara huo wa Simba ulioongozwa na pikipiki na msururu wa magari ulipofika eneo la kituo cha mabasi Ubungo ulitaka kuingia kituo kikuu cha mabasi hivyo kusababisha mtafaruku mkubwa, lakini baadaye walikubali kuonyoosha hadi Ubungo mataa na kukata kuingia barabara ya Mandela.

Mashabiki waliokuwa wakiukimbiza msafara huo kwa miguu kutoka makao makuu ya klabu ya Simba mtaa wa Msimbazi waliachwa wasijue la kufanya baada ya magari hayo kuongeza mwendo na kuwaacha nyuma eneo la Gereji barabara ya Mandela.

Msafara kutoka eneo la Gereji haukusimama tena mpaka ulipofika kwenye ukumbi wa Dar Live maeneo ya Mbagala, ambapo ulipokelewa na mamia ya mashabiki.

Nahodha wa Simba, Juma Kaseja alikuwa wa kwanza kuteremka akiwa na kombe mkononi na kuwaongoza wenzake mpaka kwenye sehemu maalum waliyokuwa wameandaliwa kwenye ukumbi huo.

Ndani ya ukumbi zilikuwa zimeandaliwa burudani mbalimbali za ngoma na muziki.

Akizungumza katika sherehe hizo, mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala alisema Simba wanatakiwa kuhakikisha wanajenga uwanja wao.

“Kutokana na historia ya Simba mlipaswa kuwa na uwanja wenu mkubwa zaidi ya ule wa Azam, pia mnatakiwa kuwa na umoja ili timu yenu  ifanye vizuri zaidi kwenye mashindano mbalimbali,”alisema Makala.

Naye makamu mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange Kaburu alisema wanataka kuandika historia kwenye mashindano ya kimataifa msimu ujao.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Posted on May 28, 2012, in Bongo, Mpira, Mpira kwa Dakika and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: