Ngassa apigwa stop Yanga


Ngasa

MSHAMBULIAJI wa Azam na Taifa Stars, Mrisho Ngassa amepigwa marufuku kujiunga na Yanga katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Ngassa ambaye tangu ajiunge na Azam miaka miwili iliyopita akitokea Yanga mara kwa mara amekuwa akihusishwa kutaka kurejea katika klabu hiyo ya Mtaa wa Jangwani na Twiga.

Akizungumza  jana jijini Mwanza, baba mzazi wa winga huyo, Khalfan Ngassa alisema hapendi kuona wala kusikia kwamba mwanaye anaondoka Azam na kujiunga Yanga.

“Sipendi wala sitarajii kuona Ngassa anahama Azam na kwenda Yanga au klabu yoyote hapa nchini kwa sababu kiwango chake cha soka pamoja na malengo yake kwa hivi sasa hayalingani na Yanga,”alisema Mzee Ngassa.

Mchezaji huyo wa zamani wa Simba na Pamba alisema, Azam ndiyo klabu pekee yenye malengo ya kukuza na kuendeleza wachezaji wake hivyo ana imani kama Mrisho ataendelea kucheza hapo atakuwa ametimiza malengo yake ya soka.

“Mrisho alikuja Mwanza kwa mapumziko baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu Bara na hata alipoitwa  kwenye timu ya Taifa alitokea hapa nyumbani,  tumezungumza mengi hususani masuala ya soka.”

“Nikamsisitizia umuhimu wa kuendelea kubaki Azam, amekubaliana nami kwamba hataondoka timu hiyo,” alisisitiza Mzee Ngassa.

Mzee Ngassa alisema mtu yeyote au mchezaji anayejua soka na mwenye malengo ya kufika mbali katika mchezo wa mpira wa miguu, lazima ataipenda Azam na atapenda kuichezea Azam, kwa sababu ndiyo timu pekee yenye malengo ya kufika mbali katika medani ya soka duniani.

Akitaja baadhi ya mambo ambayo Azam imeyafanya katika muda mfupi, ni pamoja na ujenzi wa uwanja wa mazoezi, bweni la kisasa la wachezaji wake pamoja na kutilia mkazo soka la vijana.

Alipoulizwa kuhusu kushuka kiwango kwa mwanaye tangu alipojiunga na Azam, alisema, “Mrisho hajashuka kiwango isipokuwa huo ni upepo tu katika soka na upepo huo unatokana na kuimarika kwa Ligi ya Tanzania na ubora wa timu ya Azam.”

“Mfumo wa mwalimu katika timu yao ni baadhi ya mambo yaliyomkumba Ngassa katika kipindi chote alichokuwa Azam, lakini ninakuhakikishia kwamba msimu ujao wa ligi atakuwa moto wa kuotea mbali ndani ya Azam,” alimaliza Mzee Ngassa.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Posted on May 28, 2012, in Bongo, Mpira, Mpira kwa Dakika and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: