Taifa Stars sare Yanga wakiizomea


Timu ya taifa, Taifa Stars, jana ilitoka sare ya 0-0 na Malawi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa kwenye Uwanja wa Taifa ambao wenyeji walichuniwa na mashabiki waliokuwa jukwaa la Yanga.

Kama alivyoahidi kocha mkuu mpya wa Stars Jan Poulsen juzi, timu ya taifa jana ilicheza soka la pasi fupi-fupi na ingeweza kutoka uwanjani na ushindi kama wachezaji wake wangekuwa na bahati katika mashambulizi matatu hatari zaidi waliyofanya.

Shuti la Mbwana Samata liligonga mwamba kabla ya kuokolewa katika dakika ya 58 baada ya kugongeana vizuri na kiungo-mchezesha-timu Mwinyi Kazimoto.

Haikuwa siku ya Stars kutoka uwanjani na goli katika mechi ya kwanza ya Poulsen tangu akabidhiwe mikoba katikati ya mwezi huu baada ya Shaaban Kapombe kupiga shuti lingine kali ambalo hatahivyo lilidakwa na mlinda mlango wa Malawi Simplex Nthala dakika mbili kabla ya mpira kumalizika.

Haruna Moshi alihitimisha siku mbaya mbele ya lango kwa wachezaji wa Stars mwishoni kabisa mwa mchezo baada ya kuchelewa kidogo kuuwahi mpira wa kupenyezewa na Kazimoto ambao uliwahiwa na kudakwa na Nthala.

Mashabiki wachache kwa wastani waliokuwa wamekaa jukwaa la Yanga walikuwa wakiishangilia Malawi kwa madai kuwa Taifa Stars imebagua wachezaji wa Yanga.

Kuna mchezaji mmoja tu wa Yanga — Nurdin Bakari — katika kikosi cha wachezaji 23 cha timu ya taifa, na kuna wachezaji 11 wa mahasimu Simba katika kikosi hicho.

Ukiacha mashabiki waliokuwa upande wa Yanga, hamasa ya kuingia kwenye mechi za timu ya taifa iliendelea kuwa chini tena jana baada ya majukwaa mengine yote ukiacha upande wa Simba kuwa matupu kabisa.

Habari njema kwa timu hiyo, hata hivyo, kuna uwezekano mahudhurio hayo si halisi kutokana na mkutano mkubwa wa hadhara wa chama cha upinzani cha Chadema uliofurika watu jana jioni kwenye viwanja vya Jangwani.

Licha ya suluhu hiyo, Poulsen ambaye timu yake inacheza na Ivory Coast ugenini Jumamosi katika mechi ya michuano ya awali ya Kombe la Dunia alisema timu yake ilicheza vizuri.

“Wachezaji wamecheza vizuri, timu imecheza vizuri… mwanzo mzuri. Tulikuwa na tatizo na pasi za mwisho,” alisema.

 

Chanzo: ippmedia

Advertisements

Posted on May 27, 2012, in Bongo, Mpira, Mpira kwa Dakika and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: