Yanga wamng’ang’ania bonge la kocha Ufaransa.


Yanga

JOPO la mabosi wa kamati za Utendaji, Ufundi na ile ya Usajili za Yanga, wamepitisha majina mawili ya makocha wa kigeni watakaoanza kuzungumza nao muda wowote kuanzia sasa, huku jina la Mfaransa Claude le Roy likiwamo.

Claude ambaye ana mafanikio makubwa kutokana na kuwanoa wachezaji maarufu kwenye timu zao za Taifa kama Samuel Etoo wa Cameroon na Michael Essien wa Ghana, viongozi hao wamemng’ang’ania na wamepanga kuanza kumshawishi baada ya mambo kukaa vizuri klabuni na mfanyabiashara mmoja kumwaga fedha.

Yanga haina kocha baada ya Mserbia, Kosta Papic, kumaliza mkataba wake huku msaidizi wake, Fred Minziro akibwaga manyanga. Hivyo timu hiyo inahitaji kocha wa kuiandaa kwa Kombe la Kagame linaloanza mwezi ujao jijini Dar es Salaam.

Kiongozi Mwandamizi wa Yanga aliliambia Mwanaspoti jana Ijumaa kuwa usajili wao unafanyika taratibu, lakini tayari wana majina ya makocha wawili mezani.

“Wapo makocha wawili ambao mpaka sasa tumeona watatufaa, mmoja kutoka Ufaransa ambaye kwa sasa anafundisha timu moja ya DR Congo na mwingine raia wa Uganda,”alisema kiongozi huyo huku akigoma kutaja majina yao kwa madai kuwa bado hawajafanya nao mazungumzo rasmi.

“Huyo wa Ufaransa ambaye yupo DR Congo mkataba wake unakaribia kuisha.”
Lakini Mtangazaji na Mchambuzi wa soka wa Redio Digital Congo, Papy Kumbamasaka, aliidokeza Mwanaspoti kuwa Mfaransa aliyeko DR Congo ni Claude Le Roy peke yake ambaye anafundisha timu yao ya Taifa.

“Kocha Mfaransa aliyeko hapa DR Congo ni Le Roy peke yake,” alisema Papy huku akiguna kwa madai kwamba hadhani kama Yanga itaweza kummudu kimalipo kwani ni kocha wa kiwango cha juu.

Kiongozi huyo wa Yanga alisema pia kuwa makocha waliokuwepo wamewaambia kwenye ripoti kwamba kunahitajika wachezaji wanne, mabeki wawili na mastraika wawili ambao uongozi umeridhia kufanya usajili wao kwenye Kombe la kagame mwezi ujao.

“Yule kiungo wa Uganda, Owen Kasule, tumezungumza naye, lakini ametuambia anakwenda kwanza Sudan kama akikosa mkataba kule ndiyo atarudi Yanga,”alisema kiongozi huyo.

Kocha Le Roy ana umri wa miaka 64 na uzoefu mkubwa na soka la Afrika ngazi ya timu ya Taifa kutokana na kuzinoa Ghana, Cameroon, Senegal na DR Congo.
Ameziongoza Cameroon na Senegal kwenye fainali za Afrika miaka tofauti kwa mafanikio.

Le Roy ni jina kubwa katika medani ya soka la kimataifa baada ya kuisaidia Cameroon kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1988.

Pia ndiye alimuibua Eto’o akiwa na umri wa miaka 16 na kumpa nafasi ya kuchezea timu ya taifa ya Cameroon mwaka 1997 na pia alimchezesha mechi moja ya fainali za Kombe la Dunia mwaka 1998 wakati akiwa na umri wa miaka 17.

Hiyo ilimfanya Eto’o kuwa mchezaji mdogo zaidi kucheza michuano hiyo.

Chanzo: Mwanaspoti

Advertisements

Posted on May 26, 2012, in Bongo, Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: