TFF kujadili mustakabali Yanga.


SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga kubwaga Manyanga, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kupitia Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za wachezaji inatarajiwa kutoa maamuzi kuhusiana namustakabali mzima wa klabu hiyo ambayo hivi karibuni imekuwa katika mgogoro uliosababisha viongozi kadhaa kujiuzulu.

Mbali ya Nchunga, viongozi wengine waliotangaza kujiuzulu kwa nyakati tofauti ni pamoja Makamu Mwenyekiti Davis Mosha, pamoja na wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Mbaraka Igangula, Mzee Yusuf, Mohammed Bhinda, Ali Mayay, Seif Ahmed na Pascal Kihanga.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alisema kwamba walipokea barua kutoka Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, ikiomba mwongozo baada ya kutokea kwa sintofahamu hiyo.

Alisema kwa kuzingatia hilo, TFF ilipeleka suala hilo katika Kamati yake ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji iliyo chini ya uenyekiti wa Alex Mgongolwa ili itoe maoni yake kisheria, nini kifanyike kuhakikisha Yanga inaendelea na shughuli zake kama kawaida.

Alisema, Kamati hiyo baada ya kukutana na TFF na baadaye Kamati ya Uchaguzi ya Yanga pamoja na Kamati ya Uchaguzi ya TFF, zitapewa maelekezo ya kufanya kwa kuzingatia taratibu zilizopo.

Katika hatua nyingine, Baraza la Wazee la klabu ya Yanga, limepongeza uamuzi wa Nchunga kujiuzulu na kuwa baada ya zoezi hilo wanasubiri mwongozo toka TFF ili waweze kuendelea na mchakato mwingine, ukiwemo wa kukabidhi timu kwa baraza la wadhamini ambalo litasimamia usajili wa wachezaji na mambo mengine.

Hata hivyo, baraza hilo kupitia kwa Katibu wake, Ibrahim Akilimali, lilisema kwamba, kujiuzulu kwa Nchunga kunamaanisha kuwa, hata wajumbe wengine waliogoma kuachia ngazi kama walivyowataka, nao hawawatambui kama ni viongozi wa Yanga.

Aliongeza kuwa pamoja na kujiuzulu huko, bado wanaendelea na mpango wao wa kufika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), pamoja na wizara yenye dhamana na michezo, ili kukagua mali za Yanga, kwani wanaamini kulikuwa na ubadhirifu mkubwa.

Juzi, Nchunga alitangaza kujiuzulu wadhifa wake huo kufuatia msigano baina yake na baadhi ya wanachama wa Yanga wakiongozwa na Baraza la Wazee, kumtaka ajiweke kando kutokana na kushindwa kuiletea mafanikio klabu hiyo, ambayo ilijikuta ikipokwa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliokwenda kwa mahasimu wao Simba.

Chanzo : Tanzania Daima

Advertisements

Posted on May 26, 2012, in Bongo, Mpira, Mpira kwa Dakika and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: