Mawala ang’ang’ania namba ya Nsajigwa.


BEKI wa Moro United na timu ya soka mkoa wa Ilala, Erick Mawala (19), amesema yeye ndiye mrithi halali wa nafasi ya Shadrack Nsajigwa katika kikosi cha Yanga. Kauli hiyo imeungwa mkono pia na aliyekuwa kocha wa Moro United na timu ya Ilala, Hassan Banyai.

Hivi karibuni Nsajigwa alikaririwa akisema fikra zake kwa sasa ni kwenda kumalizia soka lake kwenye kikosi cha Tanzania Prisons ya Mbeya iliyorejea Ligi Kuu Bara kabla ya kuamua kutundika daruga.

Huku mashabiki wa Yanga wakitafakari mtu wa kuziba pengo la nahodha huyo aliyecheza kwa mafanikio makubwa kwa kipindi chake chote,

Mawala aliliambia Mwanaspoti jana Ijumaa jijini Dar es Salaam akisema: “Binafsi najiamini naweza kuvaa viatu vya Nsajigwa hadi mashabiki wakamsahau.

“Siri yangu kubwa ni kujiamini, kujituma na nidhamu. Ni mambo ambayo nayazingatia sana katika soka.”

Alisema endapo Yanga watazubaa katika zoezi la kumsajili anaweza akamwaga wino wakati wowote kwenye klabu za Jeshi za JKT Ruvu au Ruvu Shooting ambazo zinapigana vikumbo kuwania sahihi yake.

Aliongeza: “Nimefuatwa na viongozi wa JKT Ruvu na Ruvu Shooting kunitaka nijisajili nao kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.”

Naye Banyai alisema: “Mawala ni mchezaji mwenye bidii na nidhamu ya mchezo, nimekuwa na Mawala kwenye timu ya mkoa wa Ilala na pia Moro. Ni beki ambaye ana uwezo mkubwa wa kumzuia adui, naamini akipewa nafasi anaweza kuwa mrithi sahihi wa Nsajigwa.”

Chanzo: Mwanaspoti

Advertisements

Posted on May 26, 2012, in Bongo, Mpira, Mpira kwa Dakika and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: