Mafisango alikuwa hana chochote kwao.


mafisango

PATRICK Mafisango alikufa bila kuacha kitu chochote nyumbani, lakini Baba Mlezi wake, Papa Pierre, amelia machozi kwani nyumba aliyokuwa amjengee mwaka huu imeyeyuka.

Mafisango ambaye alikuwa mchezaji wa Simba alifariki kwa ajali ya gari jijini Dar es Salaam hivi karibuni na kuzikwa kwao Kinshasa Jumapili iliyopita.

Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu na hali halisi mchezaji huyo hakuacha mali yoyote ile wala alikuwa hata hajajenga.

Papa Pierre ambaye ni shemeji wa Mafisango, alisema: “Mafisango alikuwa hajajiendeleza hata kidogo kwa vile kazi nyingi alifanya nje ya Kinshasa.

“Lakini nilikuwa nimezungumza naye akaniahidi kwamba nitafute kiwanja kizuri hapa mjini aje kujenga nyumba moja kubwa ya familia.

“Safari hii alikuwa aende Rwanda halafu ndiyo aje hapa Kinshasa kufanya hayo mambo, nasikitika sana kwa vile imeshindikana. Ni mapenzi ya Mungu.”

Baba mlezi huyo analala kwenye nyumba ya Shirika la Nyumba la Taifa tangu aanze kuishi na Mafisango tangu akiwa mdogo.

Kiongozi mmoja wa Simba ambaye hakupenda kutajwa jina lake aliiambia Mwanaspoti akisema: “Sisi tunashangaa sana hizo lawama tunazotupiwa, tuligharimia mambo mengi sana hapa na mpaka kusafirisha mwili wake.

“Hayo mafao mengine tunafanya utaratibu tuwape, halafu mnapaswa kujua kwamba Mafisango alishamaliza mkataba wake na Simba.

“Isitoshe sisi tulikuwa tunamlipa mshahara mnono sana na posho anapewa hata nyumba anapangiwa, pesa zake alikuwa anafuja kwenye starehe sasa sisi tufanyeje hapo?”

Chanzo: Mwanaspoti

Advertisements

Posted on May 26, 2012, in Bongo, Mpira, Mpira kwa Dakika and tagged . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: