Kocha wa Stars afagilia nyumbani


  KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesema wachezaji wanaocheza Ligi ya nyumbani ndiyo wana nafasi kubwa  katika kikosi chake kuliko wale wanaosakata soka nje ya nchi.

Kauli hiyo ameitoa jana baada ya kuridhishwa na kujituma kwa wachezaji waliopo hivi sasa kwenye  kikosi cha Taifa Stars kitakachoshuka dimbani leo jioni kucheza na Malawi katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na mechi ya kuwania kufuzu kushiriki  Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast.

Alisema timu nyingi za taifa hivi sasa zinatumia zaidi wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani kwa sababu wengi wao hujituma zaidi uwanjani tofauti na wale wanaocheza nje kwa sababu nao wanakuwa wanatafuta nafasi ya kucheza soka la kulipwa.

“Sitaangalia ukubwa wa jina la mchezaji katika kikosi changu, ninachoangalia zaidi ni uwezo na kujituma uwanjani, sababu ninachotaka ni mafanikio na siku zote mafanikio hayaji kirahisi,”alisema Kim.
Alisema,”nipo radhi katika kikosi changu kuwa na wachezaji wote wanaocheza ligi ya nyumbani endapo tu watakuwa na sifa za kuwa kwenye timu ya taifa.”

Alisema wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi wana matatizo mengi ikiwa ni pamoja na kutojituma uwanjani hivyo kutokana na hali hiyo ni kheri akatoa nafasi kwa wale wa nyumbani na wachezaji wachache wa nje ambao wanajitoa kwa ajili ya nchi yao.

Chanzo Mwananchi

Advertisements

Posted on May 26, 2012, in Bongo, Mpira, Mpira kwa Dakika and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: