Msiba wa mafisango utata…


Wake wa Mafisango

Sweetbert Lukonge na Michael Momburi
WAKATI Simba ikikiri kutopeleka mchango wa rambirambi ya msiba wa wa Patrick Mafisango yaliyefariki kwa ajali ya gari wiki moja iliyopita, hali ya maisha imekuwa ngumu zaidi nyumbani kwa marehemu baada ya kujikuta hawana kitu kufuatia kutumia zaidi ya dola 3500(Sh5.4 milioni) kwa ajili ya mazishi Jumapili iliyopita.

Kupitia Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga aliithibitishia Mwananchi kuwa, hakuna pesa ya rambirambi iliyopelekwa kwa familia ya marehemu na hiyo ni kwa sababu mpaka sasa bado haijafahamika ni nani hasa anastahili kupewa.

Kamwaga alisema wapo kwenye mchakato na wanaendelea kuwasiliana na familia kujua mpangilio wao na mfuatiliaji wa mirathi na mgawanyo mzima kabla ya kukabidhi fungu hilo ambalo hakuliweka wazi kwamba ni kiasi gani.

“Siyo kwamba tumeshindwa kutuma hizo fedha, sababu kubwa iliyofanya zoezi hilo lichelewe ni kutaka kujua watu gani hasa wanaostahili kupewa rambirambi hizo kwa sababu Mafisango hakuwa na wazazi isipokuwa tunatambua kwamba ameacha watoto watatu(Patrina, Crespo na David).

“Tupo katika mchakato wa kuangalia ni watu gani wanaostaili kupata fedha hizo na pindi mambo yatakapokuwa tayari tutakabidhi kwa wahusika,” alisema Kamwaga na kudai bado wanaendelea  kupokea michango mbalimbali kutoka kwa wadau na wapenzi wa soka nchini Tanzania na hawataweka wazi kwa watu wa nje ya familia kwasababu za kiusalama kwa wahusika.

Nchini DRC, Orly Elenga aliyekuwa akiishi na Mafisango Dar es Salaam ambaye familia imemteua kufuatilia mafao ya marehemu aliiambia Mwananchi jana kwa njia ya simu kutoka Kinshasa: “Gharama zilizotumika mpaka jana(juzi Jumanne) ilikuwa ni dola 3500 na zote ni baba ametoa mfukoni kwake na mingine wamechangia ndugu, Simba haijaleta kitu. Tulitegemea ile siku ya mazishi angalau wangetupunguzia gharama lakini hatukuona chochote, mpaka leo(jana) hakuna mawasiliano yoyote.”

“Ukweli ni kwamba hapa nyumbani maisha ni ya shida sana Baba ametumia fedha zake ambazo alikuwa amewekeza kwenye biashara yake ya mbao, ni shida sana ndugu yangu tunajaribu kuwasiliana tena na Simba tusikie lakini mimi ndiyo nimeteuliwa kufuatilia mirathi na tayari wale wake za Mafisango wamesharudi kwao na watoto pia wameondoka wanasubiri utaratibu wa kusaidia watoto wasome na kuishi,” alisema Elenga ambaye ni mtoto wa Dada ambaye ndiye mlezi wa Mafisango na msimamizi mkuu wa mirathi.

Mwakilishi wa Simba kwenye mazishi ya Mafisango yaliyofanyika Jumapili jioni jijini Kinshasa, Joseph Itangare aliitoa wasiwasi familia na kusisitiza kuwa Orly hajapewa fedha yoyote ambapo klabu inafanya utaratibu na kila kitu kitawasilishwa.

Klabu ya APR ya Rwanda na Shirikisho la Soka la nchi hiyo limeweka wazi kwamba lipo tayari kucheza mechi ya kirafiki na Simba kuchangia familia ya watoto watatu wa Mafisango ambaye amefanya kazi kubwa Tanzania na Rwanda.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Posted on May 24, 2012, in Bongo, Mpira kwa Dakika and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: